Pata taarifa kuu
ZAMBUCHAGUZI

Zambia: Uchaguzi wa urais katika hali ya mdororo wa kiuchumi

Raia wa Zambia wanapiga kura leo Alhamisi, kumchagua rais na wabunge kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitano ijayo. Rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu alichaguliwa mwezi Januari 2015, baada ya kifo cha Michael Sata, lakini uchaguzi huo ulipingwa na vyama vya upinzani.

Wagombea wawili katika uchaguzi wa urais wa Zambia: Kaimu Rais, Edgar Lungu (kushoto) na mgombea wa cham acha UPND Hakainde Hichilema (kulia).
Wagombea wawili katika uchaguzi wa urais wa Zambia: Kaimu Rais, Edgar Lungu (kushoto) na mgombea wa cham acha UPND Hakainde Hichilema (kulia). AFP PHOTO/CHIBALA ZULU-REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Wagombea tisa wanawania urais lakini ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya rais Edgar Lungu na mpinzani wake Hakainde Hichilema.

Wakati huu, baada ya kampeni iliyogubikwa na misukosuko, chama cha UPND kumebaini kwamba hakitokubali kushindwa. hayo yanajiri wakati nchi hii inakabiliwa na mdororo wa kiuchumi, usio kuwa wa kawaida. Zambia ni nchi yenye sifa ya utulivu kwa miongo kadhaa.

Hakainda Hichilema, mwenye umri wa miaka 54, ni mgombea mkuu katika upinzani kwa tiketi ya chama cha UPND, ambaye, anashindana kwa mara ya tano katika uchaguzi wa urais.

Kuelekea kwenye uchaguzi huu, kuna hali ya wasiwasi ya kuzuka kwa vurugu baada ya uchaguzi huo, ambapo wafuasi wa chama tawala na upinzani walikabiliana wiki hii.

Siku ya Jumatatu, wafuasi wa chama tawala PF cha rais Lungu waliwavamia wafuasi wa Hichilema wa chama cha UPND katika wilaya ya Mtendere jijini Lusaka walipokuwa katika mkutano wa kisiasa.

Mwezi uliopita, Tume ya Uchaguzi ilisitisha kampeni kwa muda wa siku 10 kama njia mojawapo ya kuzuia machafuko kipindi cha kutafuta kura.

Tume ya uchaguzi inasema zaidi ya wapiga kura Milioni 6 wanatarajiwa kupiga kura, kuanzia asubuhi kesho hadi jioni.

Tume ya Umoja wa Afrika kupitia sauti ya Mwenyekiti wake, Nkosazana Dlamini-Zuma, imepongeza Zambia kwa "kuandaa uchaguzi mfano na wenye mafanikio na wenye utulivu."

Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan amepewa jukumu na Umoja wa Afrika (AU) kusimamia uchaguzi huo. Kwenye Twitter, ameonyesha jukumu atakalo kuwa nalo katika uchaguzi huo, ambao unaonekana tete na wenye mvutano.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.