Pata taarifa kuu
ITALIA-SIASA

Italia: kura ya maoni ya katiba kufanyika mwezi Novemba

Mahakama Kuu ya Italia imeidhinisha saini za watu 500 000 zinahitajika ili kufanyika kwa kura ya maoni maarufu kuhusu mageuzi ya Katiba ya Italia itakayofanyika, pengine mwezi Novemba.

Matteo Renzi akizungumza na Maria Elena Boschi, Waziri wa Mageuzi ya Katiba, Septemba 1, 2014, mjini Roma.
Matteo Renzi akizungumza na Maria Elena Boschi, Waziri wa Mageuzi ya Katiba, Septemba 1, 2014, mjini Roma. REUTERS/Max Rossi/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura wataalikwa kuamua juu ya mustakabali wa Katiba inayotumika tangu 1948 na ambayo ina Ibara 139.

Kwa upande wa Waziri Mkuu, Matteo Renzi, kura ya maoni hii ni kipimo cha kisiasa tangu kuingia kwake madarakani (bila kupigiwa kura) katika Ikulu ya Chigi Februari 22, 2014.

Hadi sasa, Bunge na Baraza la Seneti vina mamlaka sawa. Kama kura ya "ndiyo" itashinda, Bunge litapigia kura imani kwa serikali na kwa wingi wa sheria. Baraza la Seneti ambalo lina wajumbe 100 tu badala ya 315, litakuwa na mamlaka ya kikanda badala ya kitaifa.

Lengo hasa ni kuhakikisha kuwepo kwa utulivu wa kisiasa, kurahisisha maisha ya kisiasa na kupunguza gharama. Kwa mujibu wa Matteo Renzi na chama chake cha Democratic, marekebisho hayo ni muhimu kwa ajili ya kufufua uchumi wa nchi. Lakini mageuzi hayo hayaridhishi vyama vya mrengo wa kulia na vuguvugu linalojulikana kwa jina la Nyota 5. Hata hivyo vyama vya mrengo wa kushoto havifurahishwi na mageuzi hayo.

Kambi inayotetea kura ya "hapana"' inaamini kwamba jukumu la Baraza mpya la Seneti halina maana yoyote na hakuna kinacho hakikisha punguzo katika matumizi. Kwa upande wa wananchi wa Italia, zaidi ya 50% hawaelewi chochote kuhusu mradi wa mageuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.