Pata taarifa kuu
UGIRIKI-EU-UCHUMI

Ugiriki: makubaliano yafikiwa juu ya mkopo mpya na madeni

Mawaziri wa Fedha kutoka nchi zinazotumia sarafu ya Euro walikutana Jumanne jioni mjini Brussels, na kufikia makubaliano juu ya kutoa mkopo mpya wa Euro bilioni 10.3 kwa nchi ya Ugiriki. Suala jingine muhimu: Mawaziri wa Fedha walikubaliana hatua ya kupunguza madeni ya Ugiriki.

Kamishna wa Ulaya mwenye dhamana na Uchumi na Fedha Pierre Moscovici (kushoto) naWaziri wa Fedha wa Ugiriki, Euclid Tsakalotos, wakati wa mkutano Mei 24, 2016 Brussels.
Kamishna wa Ulaya mwenye dhamana na Uchumi na Fedha Pierre Moscovici (kushoto) naWaziri wa Fedha wa Ugiriki, Euclid Tsakalotos, wakati wa mkutano Mei 24, 2016 Brussels. REUTERS/Eric Vidal
Matangazo ya kibiashara

Mkutano ulidumu karibu masaa 11 Jumanne jioni mjini Brussels. Mazungumzo yaliyoendeshwa kwa kasi ambayo yanakumbusha umuhimu wa mdororo wa uchumi unayoikumba Ugiriki, moja ya nchi zinazotumia sarafu ya Euro. Mapema Jumatano hii asubuhi, Waziri wa Fedha wa Ufaransa, Michel Sapin, amethibitisha kuwa mkataba umefikiwa na nchi zinazotumia sarafu ya Euro juu ya kutolewa kwa mkopo mpya kwa nchi ya Ugiriki.

Mkopo huyo mpya ni Euro bilioni 10.3. Lakini utatolewa kwa mkato, ambapo sehemu ya kwanza, sawa na Euro bilioni 7.5, itatolewa katikati ya mwezi Juni, mwandishi wetu mjini Brussels amearifu.

Kwa mujibu wa Michel Sapin, Waziri wa Fedha wa Ufaransa, huu ni ushahidi wa kurudi kwa imani kati ya nchi za Ulaya na serikali ya Ugiriki na juhudi zilizofanywa na nchi hiyo. "Makubaliano haya na majadiliano yote kati yetu yalionyesha jitihada kubwa, serikali ya Ugiriki kuwa na imani na nchi za Ulaya, uwezo wake wa kutekeleza miradi mbalimbali, hata kama ni magumu kisiasa mageuzi muhimu. Na mkataba huu kwanza ni kitendo cha imani kwa Ugiriki leo, " amesema Bw Sapin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.