Ziara ya rais wa Zimbabwe nchini China inalenga kuwakejeli viongozi wa nchi za Magharibi
Imechapishwa:
Cheza - 08:44
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili imeangazia kwa kina ziara ya rais wa Zimbabwe nchini China, ziara ambayo inalenga kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili kiuchumi.
Nchi ya Zimbabwe na China zinaushirikiano wa kihistoria kwakuwa katika miaka ya sitini nchin hiyo ilishiriki kikamilifu kuwasaidia wapigania uhuru wa Zimbabwe, safari hii rais Robert Mugabe anafanya ziara nchini humo kwa lengo la kuboresha ushirikiano huu.
Malengo ya ziara yamewekwa wazi kuwa ni pamoja na kuomba msaada toka katika taifa hili la pili kwa uimara wa uchumi duniani, je ziara hii itainufaisha Zimbabwe na kuwakejeli viongozi wa nchi za magharibi ambao wameiwekea vikwazo? Ungana nasi.