Pata taarifa kuu

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe atangaza kumuunga mkono rais wa Uganda Yoweri Museveni

Wakati serikali ya Uganda ikitangaza kwamba itafanya mazungumzo na mataifa ya Magharibi baada ya kutishia kusitisha misaada ya fedha kutokana na hatua ya rais Yoweri Museveni kutia saini mswada wa sheria unaopiga marufuku ndoa za jinsia moja nchini humo, rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amemuunga mkono rais wa Uganda kuhusu hatuwa yake hiyo ya kupinga ndoa za watu wa jinsi moja.

Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika ghafla ya sherehe ya harusi ya binti yake wa pekee, rais Mugabe amesema haki ya binadamu ni mwanamke kuolewa na mwanaume, na sio kuolewa na mwanamke mwenziye, na hii ndio uvunjifu wa haki za binadamu.

Rais Mugabe amkuwa akiwashambulia sana wahusika wavitendo vya ndoa ya jinsia moja, mara akiwaita, mmbwa, wakati mwingine nguruwe. Mugabe amesema alikuwa hajuwi kama nchini mwake kuna shirika la mashoga, na aliambiwa hivi majuzi, uchunguzi unaenda kuanzishwa kujuwa ni kinanini

Zimbabwe hairuhusu ndo za watu wa jinsia moja kama ilivyo kwa jirani yake Afrika Kusini. Sheria ya kifungo chini humo inakataza ndoa za watu wa jinsi moja, na inaagiza kifungo cha mwaka mmoja na faini.

Serikali ya Uganda imejikuta matatani baada ya kupitisha sheria inayopiga marufuku ndoa za jinsia moja.

Tayari Marekani imetangaza kusitisha msaada wake wa Uganda kufuatia hatuwa hii, huku vitisho vikiendelea kutolewa na mataifa ya magharibi juu ya hatuwa hiyo.

Serikali ya Kampala sasa inasema itaanza kubana matumizi ya fedha katika Wizara mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.