Afrika inajifunza nini kuhusu ukuaji wa uchumi wa taifa la Nigeria.
Imechapishwa:
Cheza - 08:55
Juma hili kwenye makala ya Gurudumu la Uchumi, tumeangazia sehemu ya pili ya namna ambavyo nchi ya Nigeria imefanikiwa katika kuimarisha uchumi wake kupitia sekta mbalimbali ambazo awali hazikujumuishwa kwenye ukokotoaji wake.
Mtangazaji wa makala hii, amezungumza na mtaalamu wa masuala ya Uchumi wa dunia, Daktari Honesty Ngowi ambaye pia ni mhadhiri kwenye chuo kikuu cha mzumbe nchini Tanzania.
Dr Ngowi anajaribu kueleza ni kwanini Nigeria uchumi wake umekua kwa haraka na kuelezwa kuwa miongoni mwa mataifa ambayo sasa ni tishio kiuchumi barani Afrika hali ambayo hata imeifanya nchi ya Afrika Kusini Kugutuka.
Mtaalamu huyu ameenda mbali zaidi kwa kueleza pia ni kwanini pamoja na nchi ya Nigeria kukua kiuchumi bado kiuhalisia haijaendelea kama nchi nyingine na hii anasema ni kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo.