Pata taarifa kuu
UFARANSA-NIGERIA-Diplomasia

Usalama na uchumi katika ajenda ya ziara ya rais wa Ufaransa nchini Nigeria

Rais wa ufaransa François Hollande ni mgeni wa heshma nchini Nigeria katika sherehe ya kumbukumbu ya miaka mia moja ya muungano wa taifa hilo. Ziara ya siku moja, ambayo ni ishara kubwa, kwa taifa ambalo sehemu yake kubwa linazungumza kingereza. Kando na sherehe hizo, mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, amani na maendeleo katika bara la Afrika unatazamiwa kuanza mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria.

Marais wa Ufaransa na Nigeria, Francois Hollande na Goodluck Jonathan mjini Paris, februari 11 mwaka 2013.
Marais wa Ufaransa na Nigeria, Francois Hollande na Goodluck Jonathan mjini Paris, februari 11 mwaka 2013. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Hii ni fursa ya rais wa Ufaransa ya kudumisha uhusiano, hasa katika masuala ya usalama, katika nchi ambayo inakabiliwa na vurugu za usalama zinazosababishwa na kundi la waislamu la Boko Haram.

Visa vya mashambulizi ya kujilipua, mauaji ya kuvizia, na utekaji nyara, vimekua vikishuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Nigeria, huku kundi la Boko Haram likiendelea na hujuma zake kaskazini mwa taifa hilo, baada tu ya jeshi kuanzsha operesheni tangu katikati mwa mwezi wa mei mwaka 2013 katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa.

Siku tatu ziliyopita, watu wenye silaha walifanya shambulizi dhidi ya shule moja la sekondari, na kuua wanafunzi 43 katika jimbo la Yobe. Mpaka sasa hakuna kundi lolote ambalo, limekiri kutekeleza shambulio hilo, lakini bado dhana ya mauaji hayo imekua ikielekezwa kwa kundi la Boko Haramu.

Mbali na sherehe ya kumbukumbu ya miaka mia moja ya muungano, Nigeria inaandaa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, amani na maendeleo katika bara la Afrika. Viongozi wengi wanasubiriwa kushiriki mkutano huu. François Hollande ni mmoja pekee wa marais kutoka mataifa ya magharibi, ambaye amealikwa katika mkutano huu.

Ziara hii ya rais François Hollande inakuja baada ya mwenyeji wake wa Nigeria, Goodluck Jonathan kufanya ziara mjini Paris mwezi desemba mwaka jana, ziara ambayo rais Goodluck Jonathan, aliomba Ufaransa kusaidia kuweka ushirikiano wa kimataifa kwa kukabiliana dhidi ya kundi la Boko Haram.

Juma liliyopita, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alitishia katika ukanda wa video kuanzisha mashambulizi katika jimbo muhimu la mafuta linalopatikana kusini mwa Nigeria, matamshi ambayo yaliwafanya viongozi wa taifa hilo, kutoa wito wa kuweko na ushirikiano wa kimataifa dhidi ya waasisi wa kundi hilo, ambao wako pembezuni mwa ziwa Tchad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.