Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Nigeria imewezaje kufanikiwa kiuchumi na kuwa taifa imara Afrika

Imechapishwa:

Makala ya Gurudumu la Uchumi tutaangazia Uchumi wa Taifa la Nigeria, Uchumi ambao juma hili umekuwa gumzo hapa barani Afrika na Ulaya, uchumi ambao umetajwa kukua kwa kiwango cha juu kiasi cha kuipita nchi ya Afrika Kusini, Sekta ya Filamu, mawasiliano ya simu na mafuta zikiwa miongoni mwa Sekta zilizoongoza katika kusaidia kuinua uchumi wa taifa hilo. 

Waziri wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okonjo
Waziri wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okonjo REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mfano Nollywood imeiingizia nchi hiyo kiasi cha dola bilioni 5 sawa na asilimia 1.2 ya pato ghafi (GDP). Uchumi wa taifa hili ulikuwa kwa kiasi cha dola bilioni 510 kwa mwaka 2013, kiwango ambacho kinatarajiwa kukua kwa mwaka huu.

Waasi wa kundi la MEND nchini Nigeria ambao wamekuwa wakifanya hujuma dhidi ya mabomba ya mafuta nchini humo.
Waasi wa kundi la MEND nchini Nigeria ambao wamekuwa wakifanya hujuma dhidi ya mabomba ya mafuta nchini humo. AFP

Je nchi nyingine za Afrika zinajifunza nini toka kwa nchi ya Nigeria pamoja na Sekta zinazoelezwa kuchangia uchumi wake ikiwemo filamu na mawasiliano ya simu? Ni kweli sasa Afrika imeanza kuamka kusimamia sekta muhimu kwa manufaa ya wananchi wake?

Mtangazaji wako Emmanuel Makundi amezungumza na George Gandye mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Dar es Salaam Tanzania.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.