Pata taarifa kuu
SOMALIA-MOGADISHU

Watu wenye silaha wamuua mbunge nchini Somalia

Watu wenye silaha wamemshambulia na kumuua Mbunge mmoja nchini Somalia, Kalif Jire Warfa akiwa karibu na hoteli anayoishi ikiwa ni muendelezo wa mapigano na ghasia zilizoibuka upya wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na ukame mkali. Ofisa wa Polisi nchini Somalia, Liban Mohamed amethibitisha kuuawa kwa mbunge huyo, ambapo inaelezwa kwamba watu wawili wenye silaha walimvamia na kisha kumpiga risasi na baadaye kutokomea nae kusikojulikana.

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed akihutubia moja ya kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed akihutubia moja ya kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN Photo/Aliza Eliazarov
Matangazo ya kibiashara

Mashuhuda wa tukio hilo, wamewahusisha watu hao na kundi la wanamgambo wa Al- Shabaab ambao wanapambana na serikali dhaifu, inayoongozwa na Rais Sheikh Sharrif Ahmed inayotawala sehemu ndogo tu ya taifa hilo.
 

Kundi la Al-Shabaab ni tawi la mtandao wa kigaidi duniani Al- Qaeda, linalosababisha machafuko ya kila kukicha jijini Mogadishu na kwingineko, na hivyo kuzorotesha maendeleo ya taifa la Somalia.
 

Wapiganaji hao wanashinikiza nchi hiyo kuwa ya Kiislam.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.