Pata taarifa kuu
LIBYA

Waasi nchini Libya, waliteka tena eneo la Mashariki mwa Benghazi

Waasi nchini Libya wamefanikiwa kusonga mbele na kulirejesha kwenye himaya yao, eneo la Mashariki la Jiji la Benghazi, baada ya kuwatimua wanajeshi watiifu wa Kanali Muammer Gaddafi.Kwenye mapigano hayo makali, waasi wamejigamba kuwakamata watu sitini na watatu ambao ni wafuasi wa kiongozi huyo, huku wakiendelea kutwaa maeneo zaidi kueleka Mji Mkuu, Tripoli.

Waasi nchini Libya wakitafakari juu ya mashambulizi yao.
Waasi nchini Libya wakitafakari juu ya mashambulizi yao. REUTERS/Anis Mili
Matangazo ya kibiashara

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya waasi Mustafa Al Sagazly amethibitisha taarifa hizo, baada ya kufanya mashambulizi dhidi ya ngome ya Kanali Gaddafi, kiongozi aliyeitawala Libya kwa zaidi ya miaka arobaini.
 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Msemaji wa Baraza la Mpito la Waasi Mustafa Al Sagazly, amesema hayo akiwa katika ngome ya waasi hao jijini Benghazi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.