Pata taarifa kuu

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini watuhumiwa kuwa 'mamluki'

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, Banyana Banyana, wameshtumiwa kwa kuwa na tabia kama "mamluki" na "wasaliti" kwa kukataa kucheza mechi ya maandalizi ya Kombe la Dunia (Julai 20 - Agosti 20).

Banyana Banyana ya Afrika Kusini katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012.
Banyana Banyana ya Afrika Kusini katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012. PAUL ELLIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Banyana Banyana walipaswa kukabiliana na Botswana huko Tsakane, kitongoji kilichoko takriban kilomita hamsini kusini mashariki mwa Johannesburg. Lakini walihisi kwamba uwanja huo, mchanganyiko wa nyasi na ardhi, haukuwa na viwango vyamchuano wa kimataifa na kwamba uko kwenye lazingira mabaya na kulikuwa na hatari kubwa ya kuumia.

Banyana Banyana, ambao wanakamilisha maandalizi yao ya Kombe la Dunia huko Australia na New Zealand, walikuwa wameomba kucheza mechi hii katika uwanja unaoendana na hadhi yao, kama vile Soccer City huko Johannesburg au Uwanja wa Orlando huko Soweto.

Akinukuliwa kwa sharti la kutotajwa jina na Gazeti la kila wiki la City Press, kiongozi wa ngazi ya juu wa Shirikisho la Soka la Afrika Kusini (SAFA) aliwashutumu kwa tabia ya "mamluki" na "wasaliti".

Afrika Kusini, iliyo kwenye nafasi ya 54 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, imepangwa katika Kundi G la fainali za Kombe la Dunia, pamoja na Sweden (taifa la 3 duniani), Italia (16) na Argentina (28).

Maandalizi ya Banyana Banyana pia yametatizwa na mzozo pamoja na shirikisho lao kuhusu suala la maupurupu. Wachezaji hao waliripoti kuwa kila mmoja angepokea dola 30,000 kutoka kwa FIFA, shirikisho la kimataifa linaloandaa mishuano hiyo, lakini hakuna chochote kutoka kwa shirikisho la Afrika Kusini.

"Wachezaji wanazidisha mahitaji yao," amejibu afisa mkuu wa fedha wa Safa Gronie Hluyo, akiongeza kuwa marupurupu ya FIFA yatakuwa makubwa kuliko marupurupu yoyote yaliyowahi kulipwa kwa wachezaji wa kimataifa wa Afrika Kusini, wanaume na wanawake sawa na kukumbusha kuwa mwaka 2019, wakati wa michuano ya Kombe la Dunia iliyopita iliyoandaliwa nchini Ufaransa, Banyana Banyana walipokea kila moja sawa na dola 1,500.

Ujumbe wa Afrika Kusini utasafiri kwa ndege kwenda New Zealand katika makundi mawili siku ya Jumatano na Alhamisi. Baada ya mechi ya mwisho ya maandalizi dhidi ya Costa Rica, Afrika Kusini watamenyana dhidi ya Sweden mnamo Julai 23 huko Wellington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.