Pata taarifa kuu

Jude Bellingham amejiunga na Real Madrid akitokea Borussia

NAIROBI – Real Madrid ya Uhispania imesajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mkataba wa miaka sita.

Jude Bellingham amesajiliwa na Real Madrid
Jude Bellingham amesajiliwa na Real Madrid POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Real Madrid watalipa euro 103m (£88.5m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, pamoja na nyongeza mbalimbali zinazowezekana.

Iwapo  nyongeza hizo zitaafikiwa, usajili huo unaweza kufikia euro 133.9m (£115m).

Bellingham, ambaye alianza taaluma yake katika klabu ya Birmingham City, atawasilishwa rasimi  kama mchezaji wa Real Madrid kwenye sherehe siku ya Alhamisi.

"Asante kwa kila mtu katika BVB na kwa mashabiki kwa kila kitu katika miaka mitatu iliyopita," Bellingham aliiambia tovuti ya klabu ya Dortmund.

Kiungo huyo ambaye atafikisha umri wa miaka 20 baadaye mwezi Juni, alisajiliwa na Dortmund kutoka Birmingham mwaka 2020 kwa euro milioni 25, akiichezea klabu hiyo mechi 132 na kushinda Kombe la Ujerumani mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.