Pata taarifa kuu

Karim Benzema ni mchezaji wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia

NAIROBI – Mchezaji wa zamani wa Real Madrid ya Uhispania na mshindi wa tuzo la Ballon d'Or Karim Benzema amejiunga na mabingwa wa Saudi Arabia Al-Ittihad kwa mkataba wa miaka mitatu na .

Karim Benzema amesaini mkataba na klabu ya Saudi Arabia ya Al Ittihad  Juni 6, 2023.  Al Ittihad/Handout via REUTERS THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. MANDATORY CREDIT
Karim Benzema amesaini mkataba na klabu ya Saudi Arabia ya Al Ittihad Juni 6, 2023. Al Ittihad/Handout via REUTERS THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. MANDATORY CREDIT via REUTERS - Al Ittihad
Matangazo ya kibiashara

Benzema mwenye umri wa miaka 35, alishinda mataji 25 , ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa 5 na La Liga 4 - katika miaka 14 akiwa na Madrid lakini walikubali kumwacha aondoke ukiwa umesalia mwaka mmoja kumaliza mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania.

Akiwa Madrid, mchezaji huyo alifunga mabao 354 akiwa wa pili baada ya Cristiano Ronaldo.

Ronaldo, ambaye alifunga mabao 450 ya Real, anachezea klabu nyingine ya Saudi, Al-Nassr.

Al-Ittihad inasimamiwa na kocha wa zamani wa Wolves na Tottenham Nuno Espirito Santo.

Benzema aliichezea Real mara 648 baada ya kuhama mwaka 2009 kutoka Lyon na kufunga goli lake la mwisho katika klabu hiyo, akifunga penalti katika sare ya 1-1 na Athletic Bilbao Jumapili kabla ya nafasi yake kuchukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.