Pata taarifa kuu

Benzema amesaini kujiunga na Al-Ittihad ya Saudi Arabia

NAIROBI – Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or na klabu ya Real Madrid, Karim Benzema amesaini kujiunga na Al-Ittihad ya Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka mitatu kuanzia msimu ujao, chanzo kutoka katika klabu hiyo yenye makao yake mjini Jeddah kimethibitisha.

 Karim Benzema
Karim Benzema REUTERS - HANNAH MCKAY
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii inakuja siku chache baada ya Real Madrid kutangaza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alikuwa anaondoka kwenye klabu hiyo ya Uhispania

Benzema yuko mbioni kuungana na Cristiano Ronaldo katika ufalme wa Ghuba baada ya Mreno huyo mchezaji bora wa dunia mara tano kuhamia Al Nassr kutoka Manchester United baada ya kombe la dunia mwaka jana.

Lionel Messi, ambaye anaondoka Paris Saint-Germain baada ya misimu miwili, pia amekuwa akihusishwa na kuhamia Saudi Arabia.

Lionell Messi naye pia amehusishwa na kuhamia nchini Saudi Arabia akitokea nchini Ufaransa
Lionell Messi naye pia amehusishwa na kuhamia nchini Saudi Arabia akitokea nchini Ufaransa AP - Martin Meissner

"Benzema amesaini mkataba wa uhamisho wake kwenda Al-Ittihad kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia msimu ujao," kilisema chanzo hicho.

Maafisa wakuu kutoka kwa klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia wamesafiri kwa ndege hadi Ufaransa kujaribu kupata mkataba wa kumnunua Messi baada ya Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 35 kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na PSG wikendi.

Ujumbe wa Saudi unapanga kukutana na babake Messi na wakala, Jorge, kwa lengo la kukamilisha utiaji saini huo haraka iwezekanavyo, duru ziliiambia AFP Jumapili.

Benzema alijiunga na Madrid mwaka 2009 akitokea Lyon ya Ligue 1.

Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa huenda Mbappe akachukua nafasi ya Karim Benzema aliyeondoka Real Madrid
Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa huenda Mbappe akachukua nafasi ya Karim Benzema aliyeondoka Real Madrid AP - Bernat Armangue

Alicheza mechi 647 akiwa na Madrid na ni wa pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Real akiwa na mabao 353 -- ni Cristiano Ronaldo pekee aliye na zaidi.

Ameinua Ligi ya Mabingwa mara tano, mataji manne ya La Liga na matatu ya Copas del Rey akiwa na Madrid na ndiye anayeshikilia tuzo ya Ballon d'Or ya mchezaji bora wa dunia.

Lakini baada ya msimu mzuri wa 2021-22 alipoiongoza Real kwenye Ligi ya Mabingwa, amekuwa akisumbuliwa na majeraha katika msimu uliomalizika hivi punde na ikambidi akose kampeni ya Kombe la Dunia ya Ufaransa kutokana na tatizo la paja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.