Pata taarifa kuu

Wachezaji wanaohusishwa na ligi ya Saudi Arabia

NAIROBI – Luka Modric na Hugo Lloris ni miongoni mwa wachezaji kumi wanaohusishwa na ligi ya Saudi Arabia wakiongozwa na  Lionel Messi na Karim Benzema, watu wa karibu na mazungumzo yanayowalenga wachezaji hao wamethibitisha.

Angel Di Maria wa Argentina
Angel Di Maria wa Argentina AP - Natacha Pisarenko
Matangazo ya kibiashara

Sergio Ramos, Jordi Alba, Sergio Busquets, N'Golo Kante, Angel Di Maria na Roberto Firmino pia wametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na ligi hiyo.

Taarifa hii inakuja wakati huu maofisa wa ligi hiyo ya Saudi wakiwa mjini Paris na Madrid kujaribu kumaliza mikataba ya Messi na Benzema kwa ujumla, hatua ambayo itawaruhu kujiunga na Cristiano Ronaldo katika ufalme huo wenye utajiri wa mafuta.

Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa huenda Mbappe akachukua nafasi ya Karim Benzema aliyeondoka Real Madrid
Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa huenda Mbappe akachukua nafasi ya Karim Benzema aliyeondoka Real Madrid AP - Bernat Armangue

Mamlaka ya Saudi ipo katika mawasiliano na zaidi ya wachezaji kumi wengi wao wakiwa ni wale walioshinda kombe la dunia na klabu bingwa barani Ulaya wakitarajiwa kujiunga na ligi ya Saudi msimu ujao.

Kando na Messi, orodha hiyo inajumuisha wachezaji kama vile Benzema, Ramos, Di Maria, Modric, Hugo Loris, Kante, Firmino, Alba na Busquets.

Lionel Messi amehusishwa na ligi ya Saudi Arabia akitokea PSG
Lionel Messi amehusishwa na ligi ya Saudi Arabia akitokea PSG REUTERS - CHRISTIAN HARTMANN

Licha ya kwamba wachezaji hao wamedaiwa kupewa mikataba mikubwa, watacheza katika ligi yenye ushindani mkubwa, Saudi Arabia inalenga kukamilisha uhamisho wao kabla ya msimu mpya wa ligi kuaanza tarehe 11 ya mwezi Agosti.

Kando na watu wa karibu na mazungmzo yanayodaiwa kuwa yanaendelea, afisa wa serikali ya saudi ameiambia AFP kuwa mamlaka inafanya mazungumzo na wachezaji wa tajiriba ya juu.

Christiano Ronaldo wa Al-Nassr
Christiano Ronaldo wa Al-Nassr © Marca

Kwa mujibu wa mamlaka ya saudi, hatua hii inalenga kuifanya ligi yao kuwa yenye ushindani mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.