Pata taarifa kuu

Urawa Red Diamonds kutoka Japan ndio mabingwa vilabu barani Asia

NAIROBI – Na Jason Sagini

Wachezaji wa klabu ya Urawa Red Diamonds ya nchini Japan baada ya kushinda taji la klabu bingwa barani Asia
Wachezaji wa klabu ya Urawa Red Diamonds ya nchini Japan baada ya kushinda taji la klabu bingwa barani Asia AP - Toru Hanai
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Urawa Red Diamonds kutoka Japan ndio washindi wa klabu bingwa  bara Asia baada ya kuwashinda mabingwa watetezi Al Hilal kutoka Saudi Arabia bao moja bila jibu katika mkondo wa pili wa fainali iliyochezwa Jumamosi hii.  

Bao la kujifunga la mchezaji wa Al Hilal Andre Carrillo kwenye kipindi cha pili iliiwezesha Urawa kushinda taji hilo kwa mara ya tatu mbele ya mashabiki wa nyumbani elfu 55 katika uwanja wa Saitama uliopo kaskazini mwa Tokyo.  

“Haya ni matukio ambayo sikudhani kabisa kuwa yanaweza tokea kiuhalisia. Siamini bado." alisema nahodha wa Urawa Hiroki Sakai.

Urawa Red Diamonds ya Japan ndio mabingwa ya vilabu barani Asia
Urawa Red Diamonds ya Japan ndio mabingwa ya vilabu barani Asia AP - Toru Hanai

Klabu hiyo ya Japan ililazimika kustahimili shinikizo kali kwenye kipindi cha kwanza kutoka kwa Al Hilal, ambao walikuwa wanalenga kuweka rekodi ya kushinda taji la tano na la tatu katika misimu minne. 

Mchezo ulifunguka wakati Carrillo aligeuza mpira wa kichwa kutoka kwa Marius Hoibraten wa Urawa na kuingia wavuni mwake huku kukiwa na upepo mkali katika dakika ya 48, kabla ya juhudi za walinzi wa nyuma kujaribu kurekebisha makosa na kupelekea umati kushangilia kwa fujo. 

"Walituweka kwenye presha mara kwa mara tangu mwanzo na ulikuwa mchezo mgumu," alisema mshambuliaji wa Urawa, Shinzo Koroki, ambaye aliifungia timu yake bao katika mechi ya mkondo kwanza. 

Timu hizo mbili zilikuwa zinakutana katika fainali ya ligi ya vilabu bingwa barani Asia kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka sita. Urawa ilishinda mwaka wa 2017 lakini Al Hilal iliibuka kidedea miaka miwili baadaye. 

Al Hilal walikosa huduma za nahodha Salman Al Faraj aliyejeruhiwa na winga nyota Salem Al Dawsari anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Wachezaji wa Urawa Red Diamonds ya Japan
Wachezaji wa Urawa Red Diamonds ya Japan AP - Toru Hanai

Kocha wa Al Hilal, Ramon Diaz alifanya mabadiliko matatu kwenye mechi ya mkondo wa pili, akimtoa mshambuliaji wa Mali, Moussa Marega na kumuingiza mzoefu wa Peru, Carrillo, huku Urawa ikisalia na kikosi kilicheza mechi ya raundi ya kwanza. 

Al Hilal ilipata nafasi ya mapema wakati Odion Ighalo alipopenyeza vizuri kwenye eneo la goli ila mlinzi wa Urawa Alexander Scholz alizuia shuti lake kwenye mstari wa goli. 

Michael wa Al Hilal pia manusura afunge bao kwenye kipindi cha kwanza, lakini kipa wa Urawa Shusaku Nishikawa alitoka haraka kwenye lango lake na kupangua shuti lake.

Mashabiki wa klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kabla ya mechi yao ya klabu bingwa barani Asia
Mashabiki wa klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kabla ya mechi yao ya klabu bingwa barani Asia AP - Toru Hanai

Urawa pia ilikaribia kufunga bao wakati Shinzo Koroki, ambaye aliifungia timu yake bao katika mkondo wa kwanza, alipogonga mwamba wa goli kwenye dakika ya thelathini. 

Nishikawa tena alilazimika kuwa macho kuzuia juhudi za mbali za Carrillo kipindi cha kwanza kikielekea kukamilika, kabla ya Yoshio Koizumi wa Urawa kuchomoa shuti nje ya lango ule upande mwingine. 

Wajapani walifurahia kumiliki mpira zaidi kuanzia wakati huo na Atsuki Ito nusura aongeze bao la pili alipopiga shuti nje ya lango bila golikipa kufikia shuti hilo.

Mashabiki wa mpira wakati wa mechi ya klabu bingwa barani Asia
Mashabiki wa mpira wakati wa mechi ya klabu bingwa barani Asia AP - Toru Hanai

Al Hilal walifanya mashambulizi machache sana katika kipindi cha pili na Nishikawa alikuwapo tena kumnyima Ighalo bao wakati timu ya Saudia ilitengeneza nafasi mwishoni mwa mchezo. 

Fainali hiyo ilifanyika baada ya zaidi ya mwaka mmoja baada ya msimu wa Ligi ya Mabingwa wa Asia kuanza na kucheleweshwa kwa sababu ya msimu wa baridi wa Kombe la Dunia huko Qatar na changamoto ya usafiri zilizotokana na janga la Covid. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.