Pata taarifa kuu

Gwiji wa Real Madrid Amancio Amaro amefariki

NAIROBI – Gwiji wa Real Madrid Amancio Amaro aliyepewa jina la utani 'mchawi' amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, klabu hiyo imethibitisha.

 Amancio Amaro, Gwiji wa Real Madrid
Amancio Amaro, Gwiji wa Real Madrid © Real Madrid
Matangazo ya kibiashara

Wakati akijiunga na Los Blancos akitokea  Deportivo La Coruna mnamo 1962, winga huyo wa kulia alishinda mataji tisa ya ligi na ubingwa wa Uropa  mara moja huko Madrid kabla yake kustaafu mnamo 1976.

Akiwa na Madrid, Amancio alifunga mabao 155 katika michezo 471, kabla ya kurejea kuinoa timu hiyo katika msimu wa 1984-85.

Amancio pia alichangia pakubwa wakati  Uhispania iliposhinda ubingwa wa Uropa wa 1964.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.