Pata taarifa kuu

Klabu bingwa barani Afrika : ES Setif ya Tunisia dhidi ya Al Ahly ya Misri

ES Setif ya Tunisia inamwalika bingwa mtetezi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika Al Ahly ya Misri kwa mkondo wa pili wa mechi hizo Jumamosi 14 Mei katika uwanja wa Stade du 5 Juillet.

Mashabiki wa  Wydad Casablanca ya Morocco.
Mashabiki wa Wydad Casablanca ya Morocco. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Setif wanakabiliwa na kibarua kigumu kuelekea mchuano huu baada yao kupokezwa kichapo cha magoli 4-0 kwenye mkondo wa kwanza. Al Ahly ambao pia walishinda kombe hili mwaka 2020 wanalenga kulishinda kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2006 na 2013.

Hii itakua mara ya tano kwa timu hizi kukutana huku mechi nne zilizopita zikiwa kwenye michuano ya CAF. Rekodi yao kwa sasa ni ya wastani kwani kila mmoja ameshinda mechi mbili na kutoka sare mara moja.

Al Ahly haijawahi kuandikisha ushindi katika uga wa Juillet historia wanayolenga kuifuta wanapokutana.

Kuelekea mchuano kikosi cha ES Setif kimesimama hivi Sofaine Khedeira (mlinda lango); Karim Nemdil, Hicham Belakroui, Hocine Laribi, Houri Ferhani; Ahmed Kendouci, Mohamed Khoutir Ziti, Abd El Kader Boutiche, Abderrahim Deghmoum; Akram Djahnit, Riyad Benayad.

Al Ahly wanatarajia kutumia tajiriba ya wachezaji wao wakiongozwa na  Mohamed El Shenawy (mlinda lango); Ali Maaloul, Ayman Ashraf, Yasser Ibrahim, Mohamed Hany; Walid Soliman, Hamdi Fathi, Aliou Dieng; Ahmed Abdelkader, Mohamed Sherif, Percy Tau.

Mshindi wa pambano hili atakutana na Wydad Casablanca kutoka Morocco ambao walifuzu fainali kwa jumla ya magoli 4-2 kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Petro Atletico ya Angola kwenye mkondo wa pili jana usiku.

Fainali itachezwa Mei, 30, 2022 katika uga wa Stade Mohammed V jijini Rabat nchini Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.