Pata taarifa kuu

Kufa au kupona kwa Malawi, wanawake kusimamia mchezo wa Zimbabwe na Senegal

Msikilizaji kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, mechi kati ya Zimbabwe na Guinea, itasimamiwa na wanawake.

Frank Mhango, aliifungia timu yake mabao mawili, timu yake ikitoka nyuma na kuifunga Zimbabwe magoli 2-1.
Frank Mhango, aliifungia timu yake mabao mawili, timu yake ikitoka nyuma na kuifunga Zimbabwe magoli 2-1. Pius Utomi EKPEI AFP
Matangazo ya kibiashara

Salima Mukansanga, raia wa Rwanda akitarajiwa kuwa mwamuzi wa kati, huku akisaidiwa na Carine Atemzabong raia wa Cameroon, Fatiha Jermoumi raia wa Morocco, huku msimamizi wa teknolojia ya VAR akiwa ni Bouchra Karboubi, raia wa Morocco.

Januari 10 mwaka huu, Mukansanga alitengeneza historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kusimamia mechi ya taji la AFCON, baada ya kuteuliwa kuwa mwamuzi msaidizi katika mechi baina ya Guinea na Malawi, kwenye mji wa Bafoussam.

Mchezo uliowakutanisha Senegal na Zimbabwe.
Mchezo uliowakutanisha Senegal na Zimbabwe. AFP - PIUS UTOMI EKPEI

Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International, ilizungumza na mchambuzi wa michezo George Ambangile, ambaye pia ni mchambuzi katika kituo maarufu cha redio nchini Tanzania, Wasafi FM, ambapo alizungumzia hili.

Mimi sioni ajabu sana, kwasababu hata katika ligi nyingine mbalimbali kuna wanawake wakipewa jukumu la kuwa waamuzi, katika mechi mfano katika Bundasliga nimewahi kuona, hata hapa Tanzania tunaona akina mama wanapewa nafasi.

Hata hivyo harakati zimeendelea barani Afrika kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujitokeza katika kushika nafasi mbalimbali kwenye soka mbali na kuwa waamuzi.

Sijui kwanini, lakini labda inawezekana ni kutokana pia na jamii tunazoishi, labda tunaamini Zaidi mchezo wa mpira wa miguu ni kwaajili ya wanaume tu, inawezekana ikawa sabahbu hiyo.

 

Sioni kama kuna sababu nyingine yoyote, kwasababu huu mchezo ni ajira kama ajira nyingine, ukiufanya huu mchezo hauufanyi kujifurahisha tu, unaufanya pia unaingiza kipato.
Sadio Mane, mshambuliaji wa Senegal
Sadio Mane, mshambuliaji wa Senegal Pius Utomi EKPEI AFP

Katika hatua nyingine, Rais wa Malawi, lazarus Chakwera, ameahidi kutoa Kwacha milioni moja sawa na dola za Marekani elfu 1 na 200 kwa kila mchezaji ikiwa timu hiyo itafanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Senegal.

 

Mechi kati ya Malawi na Senegal, ambayo ni ya mwisho kukalilisha mechi za kundi B, ni muhimu kwa timu zote ambapo yeyote atakeibuka mshindi ana nafasi ya kutinga hatua ya mtoano.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, rais Chakwera amesema ikiwa timu hiyo itafanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, atatoa dola elfu kwa kila mchezaji atakaecheza hivi leo na dola 500 kwa wachezaji watakaokuwa nje.

Malawi katika kundi B inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 3, nyuma ya Senegal na Guinea zenye alama 4, Guinea ikihitaji ushindi dhidi ya Zimbabwe kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.

Malawi nchi taifa pekee kutoka kusini mwa nchi za Afrika na Ukanda wa SADC, yenye nafasi ya kuingia hatua ya 16 bora ikiwa itaifunga Senegal, wakichagizwa na ushindi walioupata dhidi ya Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.