Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA 2022

Soka: Mwaka mmoja kuelekea kombe la dunia nchini Qatar

Ni mwaka mmoja kuelekea michuano ya kombe la dunia katika mchezo wa soka nchini Qatar mwaka 2022.

Uwanja wa Al-Rayyan nchini Qatar utakaokuwa mwenyeji wa baadhi ya mechi za kombe dunia 2022
Uwanja wa Al-Rayyan nchini Qatar utakaokuwa mwenyeji wa baadhi ya mechi za kombe dunia 2022 Karim JAAFAR AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandalizi yamefika katika hatua ya lala salama, ikiwa ni pamoja na viwanja kuwa tayari na miundo mbinu mingine  muhimu kama makaazi ya wageni.

Mashabiki zaidi ya  Milioni 1 kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, wanaotarajiwa kuhudhuria michuano hiyo ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza nchini Qatar.

Tarehe 21 mwezi Novemba mwaka 2022, jiji la Doha litakuwa mwenyeji wa mashindano haya makubwa duniani, pamoja na miji mingine kama Lusail, Al Khor, Al Rayyan na Al Wakrah.

Qatar iliingia kwenye historia ya mchezo wa soka duniani  mwaka 2010 baada ya kuishinda Marekani kuwa mwenyeji wa kombe la duniai, katika mazingira ambayo yalidaiwa kuwa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati ilinunua kura ili kushinda nafasi hiyo.

Mataifa 32 yatashiriki katika michuano hiyo, bara la Afrika likiwakilishwa na mataifa matano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.