Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini: Mashabiki wa soka waliopata chanjo kuangalia mechi bure

Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limetangaza kwamba watu waliochanjwa dhidi ya virusi vya Corona wataruhusiwa kuangalia mechi bure mwezi ujao, na hivyo kubaini kwamba litatoa tiketi za bure kwa watu hao kushuhudia mechi za kufuzu kombe la dunia kati ya timu ya Afrika Kusini (Bafana Bafana), na Ethiopia.

Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limetangaza kwamba watu waliopewa chanjo dhidi ya virusi vya Corona wataruhusiwa kuangalia mechi bure mwezi ujao kati ya BAfana Bafana na Ethiopia.
Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limetangaza kwamba watu waliopewa chanjo dhidi ya virusi vya Corona wataruhusiwa kuangalia mechi bure mwezi ujao kati ya BAfana Bafana na Ethiopia. rfi
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka nchini Afrika limesema, mashabiki waliochanjwa dhidi ya virusi vya Corona watapewa kipaumbele katika mechi na matukio mengine ya kiburudani.

Kufikia sasa watu milioni 10 ndio wamepokea chanjo ya virusi vya Corona wakati serikali inahitaji kuwafikia watu Milioni 40.

Serikali ya Afrika ya kusini imekuwa ikiongeza juhudi katika kuwahamasisha watu kupata chanjo, lakini wengi wanaonkana kususia kampeni ya chanjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.