Mabingwa wa zamani kuanza kusaka ubingwa wa soka barani Ulaya
Mechi za kundi ngumu la F, kuwania taji la soka barani Ulaya zinachezwa siku ya Jumanne.
Imechapishwa:
Mabingwa watetezi Ureno watafungua dimba dhidi ya Hungary, huku mabingwa mabingwa wa zamani, Ufaransa na Ujerumani wakipangwa kukutana katika mechi ya pili.
Siku ya Jumatatu usiku, katika mechi za kundi E, Slovakia walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Poland, huku Uhispania na Sweden zikimaliza mchuano wao bila kufungana.
Slovakia wanaongoza kundi lao kwa alama tatu, huku Uhispania na Sweden zikiwa na alama moja. Poland haina alama yoyote mpaka sasa.
🇸🇪 Berg scoops over from close range 😮#EURO2020 pic.twitter.com/pAsdGGjVyh
— UEFA EURO 2020 (@EURO2020) June 14, 2021
Mechi moja ya kundi D pia ilichezwa Jumatatu usiku, baada ya Jamhuri ya Czech kupata ushindi wa mabao 2-0.
Kundi la D linaongozwa na Jamhuri ya Czech ambayo ina alama tatu, sawa na Uingereza.
Croatia na Scotland, hazina alama yoyote.
Ratiba, Jumatano Juni 16 2021
Finland vs Urusi
Uturuki vs Wales
Italia vs Uswizi