Pata taarifa kuu
AFCON 2022-CAMEROON

AFCON 2022: Mechi kati ya Sierra Leone na Benin yahairishwa tena

Mechi ya mwisho kufuzu kucheza kwenye fainali ya kuwania  taji la mataifa ya Afrika mwaka 2022 nchini Cameroon, kati ya Sierra Leone na Benin, iliyotarajiwa kuchezwa siku ya Jumatatu, nchini Guinea sasa itachezwa Jumanne baada ya mvutano kuzuka kuhusu matokeo ya vipimo vya maambukizi ya Covid 19.

Mashabiki wa soka barani Afrika
Mashabiki wa soka barani Afrika Pierre Rene-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mvutano huo ulizuka baada ya Sierra Leone kukataa majibu ya wachezaji wake sita kuambukizwa virusi hivyo, na kusabababisha majibizano yaliyochelewesha mechi hiyo, kwa mujibu wa afisa waShirikisho la soka barani Afrika CAF.

Hii ni mara ya pili kwa mechi hiyo ya kundi L kuahirishwa, mwezi Machi Benin nayo ilikataa kucheza baada ya kukataa matokeo ya wachezaji wake watano kupatikana na maambukizi hayo.

Kufuzu, Sierra Leone inahitaji ushindi wa bao 1-0 au kupata mabao zaidi ya mawili iwapo watafungwa bao moja, lakini Benin wanahitaji sare ili kufuzu.

Mechi hii inachezwa mjini Nongo nchini Guinea kwa sababu, uwanja wa Freetown haukidhi maharti ya kimataifa kuandaa mechi hiyo.

Mataifa mengine 23 yaliyofuzu ni pamoja na wenyeji Cameroon, mabingwa watetezi Algeria, mabingwa mara saba Misri.

Mataifa mengine yaliyofuzu ni pamoja na, Burkina Faso, Cape Verde, Comoros, Equatorial Guinea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, Senegal, Sudan, Tunisia na Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.