Pata taarifa kuu
CAF-SENEGAL-MARK SALLY

Mchezaji yupi atatwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika?

Shirikisho la Kandanda Afrika CAF, Jumanne ijayo, Januari 9 litatoa tuzo  za wanasoka wa Afrika waliofanya vizuri mwaka 2018.

Mohammed Salah alinyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka jana.
Mohammed Salah alinyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka jana. GOAL.COM
Matangazo ya kibiashara

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo itafanyika katika Jiji la Dakar nchini senegal na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na michezo akiwemo rais wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA, Gian Infantino, Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Fatma Samoura, rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad na wajumbe wa kati ya utendaji ya shirikisho hilo.

Viongozi wa kisiasa watakaoshuhudia tukio hilo ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika na rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Liberia na mchezaji wa zamani wa kandanda, George Weah na Rais wa Senegal Mark Sally.

Baadhi ya tuzo zinazowaniwa ni ile ya mchezaji bora wa kiume ambako mshindi wa mwaka jana, Mohammed Salah anachuana na mchezaji mwezake wa Liverpool Sadio Mane na nyota wa Arsenal na timu ya Taifa ya Gabon, Pierre Emerick Aubemeyang. Salah alishinda tuzo hiyo mwaka jana.

Kwa upande wa wanawake tuzo inawaniwa na mshindi wa mwaka jana Asisat Oshoala wa Nigeria, Fransisca Ortega wa Nigeria na Thembi Kgatlana wa Afrika kusini ambaye alikuwa mfungaji bora wa fainali za Afrika za mwaka 2018 zilizofanyika nchini Ghana.

Tuzo ya kocha bora inawaniwa na kocha wa Timu ya Taifa ya Morocco, Herve Renard, Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal, Aliou Cisse na Kocha wa klabu ya Esperance ya Tunisia, Maine Chaban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.