Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO-COSAFA

Philip Chiyangwa kuendelea kuongoza COSAFA

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Zimbabwe Philip Chiyangwa, atasalia kuongoza Shirikisho la mchezo huo katika nchi za Kusini mwa bara la Afrika COSAFA.

Chiyangwa alijizolea umaarufu barani Afrika, baada ya kusaidia kuchaguliwa kwa rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad.
Chiyangwa alijizolea umaarufu barani Afrika, baada ya kusaidia kuchaguliwa kwa rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu, umechukuliwa na uongozi wa COSAFA kwa sababu sheria haimzuii kushikilia nafasi hiyo, licha ya kutokuwa rais wa soka nchini mwake.

Chiyangwa ambaye alijizolea umaarufu barani Afrika, baada ya kusaidia kuchaguliwa kwa rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad, alishindwa wakati wa Uchaguzi wa urais wa Shirikisho la soka nchini humo jijini Harare, Jumapili iliyopita.

Rais mpya wa soka nchini Zimbabwe ni Felton Kamambo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.