Pata taarifa kuu

Mashindano ya Olimpiki: Brazil yatwaa ubingwa wa mchezo wa soka kwa vijana

Brazil ndio mabingwa wa mchezo wa soka kwa vijana, katika mashindano ya Olimpiki ambayo yamemalizika nchini Argentina. Kulingana na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, mashindano hayo yalikuwa ya kuvutia katika mji wa kupendeza wa Buenos Aires.

Sherehe hizo za kufunga mashindano hayo katika uwanja wa Maracana pia zilimaanisha kutimiza jukumu rasmi la kutia saini hatua ya kupokeza bendera kwa Japan itakayoandaa mashindano yajao ya Olimpiki katika majira ya kiangazi ya mwaka 2020.
Sherehe hizo za kufunga mashindano hayo katika uwanja wa Maracana pia zilimaanisha kutimiza jukumu rasmi la kutia saini hatua ya kupokeza bendera kwa Japan itakayoandaa mashindano yajao ya Olimpiki katika majira ya kiangazi ya mwaka 2020. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Brazil walinyakua medali ya dhahabu kwa kuifunga Urusi mabao 4-1, miaka miwili baada ya kushindwa kwa mabao 7-1 katika fainali ya kombe la dunia na kuwahuzunisha mashambiki wengi katika taifa hilo.

Hata hivyo, michezo hiyo pia ilikuwa na kumbukumbu kwa wanariadha kutoka Brazil na wale wa nchi nyingine kote ulimwenguni.

Wachezaji wa Misri nao walifanikiwa, kunyakua medali ya shaba, baada ya kumaliza wa tatu.

Katika mechi ngumu, vijana kutoka Misri waliwashinda wenyeji Argentina mabao 5-4.

Mwanasakarasi wa Marekani, Simone Biles, alijishindia dhahabu 4, mwogeleaji Michael Phelps akaongeza nishani nyingine 5 na Usain Bolt akiwa ni mkimbiaji bora zaidi duniani akijishindia nishani 3 za dhahabu siku chache kabla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa atakapohitimu miaka 30.

Sherehe hizo za kufunga mashindano hayo katika uwanja wa Maracana pia zilimaanisha kutimiza jukumu rasmi la kutia saini hatua ya kupokeza bendera kwa Japan itakayoandaa mashindano yajao ya Olimpiki katika majira ya kiangazi ya mwaka 2020.

Kuna matumaini kwamba mashindano ya Japan yatakuwa bora zaidi kuliko yalivyokuwa nchini

Brazil lakini pia kuna wasiwasi kwenye nchini Japan iwapo mashindano hayo yatazidi kusambaratisha uchumi wa nchi hiyo ambao umekuwa ukijikokota kwa miaka mingi.

Senegal itakuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki kwa vijana, itakayofanyika jijini Dakar mwaka 2022.

Hatua hii imechukuliwa na viongozi wa Kamati ya michezo hii IOC, waliokutana jijini Buenos Aires, nchini Argentina.

Senegal ilipata nafasi hiyo baada kuyashinda mataifa mengine ya Afrika kama Bostwana, Nigeria na Tunisia.

Rais wa IOC Thomas Bach amesema, bara la Afrika limeungana na Senegal kufanikisha mashindano hayo, yatakayofanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Dakar litakuwa jiji la tano kuandaa michezo hii tangu kuzinduliwa kwake jijini Singapore mwaka 2010, Nanjing nchini China mwaka 2014, Buenos Aires mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.