Pata taarifa kuu
SOKA-AFCON 2017

Mali kujaribu kutetea taji la vijana dhidi ya Ghana siku ya Jumapili

Mali na Ghana zitachuana siku ya Jumapili katika fainali ya mchezo wa soka kutafuta ubingwa wa bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17.

Kipa wa timu ya taifa ya Mali Youssouf Koita
Kipa wa timu ya taifa ya Mali Youssouf Koita cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itapigwa katika uwanja wa l'Amitie jijini Libreville nchini Gabon.

Ghana ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuishinda Niger mabao 6-5 kupitia mikwaju ya penelti baada ya kumalizika kwa mchuano huo kwa muda wa kawaida kwa kutofungana.

Mali nayo iliilemea Guinea kwa ushindi wa mabao 2-0 baada ya kumalizika pia kwa kutofungana katika muda wa kawaida.

Ghana iliyokuwa imepangwa pamoja na Guinea,Cameroon na wenyeji Gabon, ilianza kampeni yao kwa kuifunga Cameroon mabao 4-0 na baadaye kuichabanga wenyeji Gabon mabao 5-0.

Mechi ya mwisho ilitoka 0-0 na Guinea. Ghana ilifunga mabao 9 lakini haikufungwa bao lolote.

Mali iliyofungwa mabao mawili katika kundi la B, ilianza kwa kutofungana na Tanzania, lakini mechi yake ya pili iliishinda Niger mabao 2-1.

Mechi ya mwisho, dhidi ya Angola, vijana wa Mali walipata ushindi mkubwa wa mabao 6-1.

Ghana inakwenda katika fainali hii ikiwa na historia ya kushinda taji hili mara mbili mwaka 1995 na 1999. Mali wameshinda mara moja mwaka 2015.

Mchuano wa fainali hata hivyo utatanguliwa na mchuano kati ya Niger Guinea kutafuta mshindi wa tatu.

Mali, Guinea, Niger na Ghana zimefuzu pia katika fainali ya kombe la dunia kwa vijana itakayofanyika mwezi Oktoba nchini India.

Michuano ijayo itafanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.