Pata taarifa kuu
CAMEROON-SOKA

Hugo Broos asema hana mpango wa kuondoka Cameroon

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon Hugo Broos anasema anataka kuendelea kufunza soka nchini humo.

Kocha Hugo Broos wakati wa michuano ya AFCON nchini Gabon mwezi Januari mwaka 2017
Kocha Hugo Broos wakati wa michuano ya AFCON nchini Gabon mwezi Januari mwaka 2017 Reuters / Amr Abdallah Dalsh Livepic
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja wiki moja baada ya raia huyo wa Ubelgiji kusema kuwa anafikiria kuachana na Cameroon.

Broos alitishia kujiondoa kwa kile alichosema ni uongozi mbaya katika Shirikisho la soka nchini humo lakini pia kutolipwa mshahara wake kwa muda mrefu.

Aidha, amekanusha madai kuwa aliomba kazi ya kuifunza timu ya taifa ya soka ya Ghana.

Kocha huyu ameonekana kubadilisha msimamo wake baada ya kukutana na Waziri wa Michezo nchini humo.

“Sitaki kuondoka Cameroon,” alisema Broos mwenye umri wa miaka 64.

“ Kama ningekuwa nia ya kuondoka nchini Cameroon ningekuwa nimeshafanya hivyo muda mrefu sana,” alisisitiza kocha huyo.

Broos ambaye amewahakikishia wapenzi wa soka nchini Cameroon kwamba hajaomba kazi nchi nyingine.

Anakumbwa sana kuisaidia Indomitable Lions kushinda taji la bara Afrika mwaka 2017 mwezi Januari nchini Gabon.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.