Pata taarifa kuu
SOKA-COSAFA

Umeme wasababisha kusitishwa kwa mchuano kati ya DRC na Comoros

Mchuano wa soka kutafuta mshindi wa Kundi D kufuzu kutafuta ubingwa wa taji la Kusini mwa Afrika COSAFA kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 kati ya DR Congo na Comoros uliahirishwa baada ya umeme kukatika nchini Afrika Kusini.

Nembo ya michuano ya COSAFA ya vijana wasiozidi miaka 20
Nembo ya michuano ya COSAFA ya vijana wasiozidi miaka 20 Cosafa.com
Matangazo ya kibiashara

Umeme ulikatika katika dakika 65 kipindi cha pili katika uwanja wa Moruleng wakati vijana wa DRC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0.

Nathan Lusuki na Ernest Sita ndio waliofungia DRC mabao hayo kabla ya mchuano huo kusitishwa baada ya umeme huo kukatika.

Kikosi ya vikiso viwili:

Comoros : Aboubacar Kaou, Said Hicham, Ali Moughni, Youssouf Habib, Mhadjou Hamza, Abadallah Boina, Kassim Hadji, Naimdine Antoisse, Abdou Hachim, Youdna Toiha, Anli Mohamed.

DR Congo : Kama Kamalanduaka, Chadrack Lukombe, Ernest Sita, Rachidi Kuamanbu, Djemes Mudiadia, Glody Mujinga, Nathan Lusuki, Tresor Yamba, Peter Zulu, Rosy Kinkela, Batista Adongba

Zambia na Malawi zinasubiri mshindi wa kwanza na wa pili katika kundi D ambayo ina DRC, Msumbiji na Comoros.

Michuano ya kutamatisha hatua ya makundi Desemba 12 2016:-

Kundi A

  • Lesotho vs Swaziland
  • Bostwana vs Afrika Kusini

Kundi C

  • Sudan vs Ushelisheli
  • Mauritius vs Angola
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.