Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

Mwisho wa mbio za Joseph Blatter

Jumatatu hii Desemba 5, Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) imeamua kiendelea kushikilia hukumu ya miaka sita ya kusimamishwa kwa rais wa zamani wa FIFA, Joseph Blatter, katika shughuli ya aina yoyote inayohusiana na soka. Raia huyo wa Uswisi hatapata bahati ya kupunguziwa adhabu kama Michel Platini.

Rais wa zamani wa FIFA Joseph Blatter mjini Lausanne Agosti 25, 2016.
Rais wa zamani wa FIFA Joseph Blatter mjini Lausanne Agosti 25, 2016. REUTERS/Pierre Albouy
Matangazo ya kibiashara

Hatma katika ulimwengu ya soka wa rais wa zamani wa FIFA Joseph Blatter imejulikana Jumatatu hii Desemba 5 mjini Lausanne, Uswisi, katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo. Hukumu ya kusimamishwa kwa miaka sita dhidi ya rais wa FIFA aliyetimuliwa kwenye wadhifa wake imeendelea kushikiliwa.

Bw Blatter amesema kuwa amepokea uamuzi huo kwa shingo upande. "Ninapokea uamuzi huo jinsi ulivyo na sintokata rufaa. Sitaki kukabiliana dhidi ya watu wasioeleweka, nina majukumu mengine, hususan afya yangu ambayo iko sawa, familia yangu na miradi mingine, " amesema Bw Blatter. Nimejifunza mengi katika soka, unaweza kushinda, lakini pia unaweza kushindwa, " ameongeza Bw Blatter.

Joseph Blatter alisimamishwa mwezi Desemba 2015 na mahakama ya ndani ya Shirikisho la Kimataifa la Soka kufuatia malipo yaliyozua utata ya Euro milioni 1.8 kwa Michel Platini, rais wa zamani wa UEFA, ambaye pia alisimamishwa. Mhakama ya juu ya michezo imeendelea kushikilia hukumu hiyo kwa Joseph Blatter wakati ambapo hukumu ya Michel Platini ilipunguzwa kutoka miaka 6 hadi miaka 4.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.