Pata taarifa kuu
EURO 2016

Ibrahimovic ataisaidia Sweden kufika robo fainali

Mchezaji mkongwe raia wa Sweden, Freddie Ljungberg amesema kuwa nchi yake inaweza kuvuka hatua ya makundi ya michuano ya Ulaya kutoka kwenye la kifo ililomo, ambapo mchezaji Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kucheza michuano yake ya mwisho ya Ulaya.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic REUTERS/Stephane Mahe
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha kocha Erik Hamren kinatarajiwa kuanza kampeni yake ya kusaka taji la Ulaya kwenye michuano ya mwaka huu June 13 kwenye dimba la Stade de France ambapo itakabiliana na Jamhuri ya Ireland.

Sweden iko kwenye kundi moja sambamba na Ubelgiji na Italia kwenye kundi E.

Timu ya taifa ya Sweden itaongozwa na mchezaji anayepewa sifa nyingi kwa sasa kwenye kikosi hicho, Zlatan Ibrahimovic, ambaye alimaliza kuitumikia timu yake ya Paris Saint Germain na anahusishwa na kutaka kujiunga na klabu ya Manchester United ya Uingereza.

Zlatan Ibrahimovic akiwa kwenye mazoezi na timu yake nchini Ufaransa
Zlatan Ibrahimovic akiwa kwenye mazoezi na timu yake nchini Ufaransa REUTERS/Stephane Mahe

Ljungberg anasema kuwa, Ibrahimovic ni mchezaji mkubwa kwenye timu na wengi wanamtegemea kumuona anafunga mabao mengi kwenye michuano ya mwaka huu. Amesema Ljungberg mchezaji wa zamani aliyeitumikia timu yake kwenye mechi 75 na aliwika kwenye fainali za mwaka 2008.

Kwa sasa Ibrahimovic amefunga mabao 62 katika mechi 112 ambazo ameichezea timu yake ya taifa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na West Ham, amesema Ibrahimovic kutokana na uchezaji wake wa nguvu, ataisaidia Sweden kutinga hatua ya mtoano kama walivyofanya mwaka 2004 ambapo walifika hatua ya robo fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.