Pata taarifa kuu
CAF-ZIMBABWE-ZAMBIA-SOKA

CAF: Zimbabwe wachuana na Zambia

Michuano ya mzunguko wa mwisho mchezo wa soka kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa upande wa wanawake inachezwa kuanzia Jumatano hii.

Nchini Congo-Brazzaville, Nzango, ni mchezo wa wanawake na wasichana unaochezwa wakiimba
Nchini Congo-Brazzaville, Nzango, ni mchezo wa wanawake na wasichana unaochezwa wakiimba Source : https://www.youtube.com/
Matangazo ya kibiashara

Makala 12 ya mashindano haya yatafanyika nchini Cameroon kati ya tarehe 19 na tarehe 3 mwezi Desemba mwaka huu wakati wa michuano hiyo.

Mataifa nane ikiwemo wenyeji Cameroon yatashiriki katika michuano hiyo.

Leo, Jumatano Zimbabwe wanamenyana na Zambia, Tunisia na Ghana huku Mali wakiwa wenyeji wa Equitorial Guinea.
Siku ya Alhamisi,Misri watakuwa nyumbani kuchuana na Cote d'Ivoire.

Warembo wa Algeria nao watakuwa nyumbani kupambana na wenzao kutoka Kenya siku ya Ijumaa, huku Senegal wakipepetana na Nigeria.

Boswatana na Afrika Kusini nao watachuana siku ya Jumamosi.

Ratiba ya michuano ya marudiano:-

Aprili 10 2016:- Zambia vs Zimbabwe

Equitorial Guinea vs Mali

Aprili 11, 2016: Ivory Coast vs Misri

Aprili 12, 2016: Kenya vs Algeria

Ghana vs Tunisia

Nigeria vs Senegal

Afrika Kusini vs Botswana

Mshindi wa michuano hii itakayochezwa nyumbani na ugenini atafuzu katika fainali hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.