Pata taarifa kuu
MOROCCO-RENARD-KOCHA-SOKA

Morocco: Mfaransa Hervé Renard kocha mpya wa Simba

Mfaransa Hervé Renard ameteuliwa rasmi kocha mpya wa timu ya taifa ya Morocco. Kocha wa zamani wa Zambia, Angola na Côte d’Ivoire anapewa nafasi kubwa ya kuwapatishi ushindi Simba wa Atlas katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017 na katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mfaransa Hervé Renard
Mfaransa Hervé Renard DENIS CHARLET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hervé Renard amerudu barani Afrika. Mfaransa huyo, mshindi wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012 alipokua meneja wa timu ya taifa ya Zambia na AFCON 2015 alipokua kocha wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire ni kocha mpya wa timu ya taifa ya Morocco. Uteuzi wake umetangazwa rasmi Jumanne hii Februari 16, 2016 mjini Rabat, katika mkutano na waandishi wa habari uyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF).

Hervé Renard anachukua nafasi ya mtangulizi wake Badou Zaki, raia wa Morocco. Zaki aliombwa kuondoka na Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), Februari 10, 2016. Shirikisho hili lilibaini kwamba kazi ya kipa wa zamani wa Simba wa Atlas haikuzaa matunda kwa timu ya taifa ya Morocco.

"Nampongeza kocha wa zamani"

Hervé Renard anapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika suala la mchezo na matokeo kuliko mtangulizi wake. Ana kai kubwa hasa ya kuitafutia ushindi timu ya taifa katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017, kisha katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

"Nina furaha kubwa kuona nimeteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Morocco, amesema kocha Renard. Tuna ratiba ndefu. timu hii inajiunga katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017, kwa sababbu ilishinda mechi zake mbili za kwanza. Kwa hivyo nampongeza kocha aliyetangulia kwa kazi nzuri aliofanya. Tunapaswa kuendelea katika njia hii, kwa matumaini kwamba soka ya Morocco inaweza kufikia katika ngazi ya juu barani Afrika, na pia kuwakilisha bara la Afrika katika Kombe la Dunia. "

Soka ya Morocco katika ukosefu wa matokeo

Morocco, ambayo ilikuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia na ambayo ina nia ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la mwaka 2026, imeendelea kupata matokeo yenye mchanganyiko kwenye uwanja wa michezo.

Hervé Renard atasaidiwa katika kazi hii na msaidizi wake mwaminifu, Patrice Baumelle pamoja na Morocco Mustapha Hadji, kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.