Pata taarifa kuu
CAF-RWANDA-SOKA

Ujumbe wa CAF mbioni kuizuru Rwanda

Wajumbe wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, wanatarajiwa kuwasili nchini Rwanda kuthathmini tena maandalizi ya nchi hiyo kuelekea fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka katika vlabu vya nyumbani CHAN.

Mji wa kigali ambako watapolkelewa wajumbe wa CAF, ambo wako mbioni kutembelea viwanja na hoteli mbalimbali, kwa maandalizi ya michuano ya CHAN.
Mji wa kigali ambako watapolkelewa wajumbe wa CAF, ambo wako mbioni kutembelea viwanja na hoteli mbalimbali, kwa maandalizi ya michuano ya CHAN. RFI/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Rwanda inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya Afrika kati ya Januari tarehe 16 hadi Februari tarehe 7 mwaka ujao wa 2016.

Wajumbe hao wa CAF watakuwa nchini Rwanda kati ya tarehe 23 hadi 28 mwezi huu na kuchunguza hoteli zitakazotumiwa na wageni wakati wa michuano hiyo pamoja na viwanja vitakavyotumiwa.

Almamy Kabele Camara naibu rais wa CAF, anatarajiwa kuongoza wajumbe wenzake kuzuru viwanja vya Amahoro, Huye na Umuganda katika wilaya ya Rubavu vinavyotarajiwa kufanyika kuandaa michuano hiyo.

Mataifa 15 yatakayofuzu katika fainali hiyo yatabainika baada ya kumalizika kwa michuno ya kufuzu mwezi Oktoba.

Mara ya kwanza kufanyika kwa michuano hii ilikuwa ni mwaka 2009 nchini Cote d'Ivoire ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa bingwa.

Makala ya pili yalifanyika mwaka 2011 nchini Sudan, huku yale ya tatu yakifanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.