Pata taarifa kuu
SOKA-TANZANIA-AFCON

Taifa Stars yaingia kambini

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini leo Jumatano jijini Dar es salaam kuanza maandalizi ya mchuano dhidi ya Misri kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars. Online
Matangazo ya kibiashara

Tanzania itaanza safari ya kutafuta tiketi kwenda Gabon ugenini katikati ya mwezi ujao dhidi ya mabingwa hao wa zamani “ Pharaon” kabla ya kuwakaribisha Nigeria mwezi Septemba jijini Dar es salaam.

Taifa Stars ambayo ilifuzu katika michuano ya Afrika mara ya mwisho mwaka 1980, imejumuishwa katika kundi moja na Nigeria, Misri na Chad.

Kocha Mart Nooij aliyepewa nafasi nyingine na uongozi wa TFF kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya vizuri katika michuano ijayo hasa kufuzu katika michezo ya CHAN itakayofanyika mwakani nchini Rwanda tayari amewaita wachezaji kwa maandalizi ya michuano hiyo.

Nooij, amewaita wachezaji 16 kuingia kambini na kitu cha kwanza kinachofanyika siku ya Jumatano ni kwa wachezaji hao kupimwa afya zao na kujua maandeleo yao kabla ya kuwajumisha katika kikosi cha pamoja kitakachokua kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji walioitwa kuingia kambini ni pamoja na , Mohamed Hussein, Peter Manyika, Hassan Isihaka, Jonas Mkude (Simba SC), Salum Telela, Juma Abdul, Nadir Haroub (Yanga SC), Aishi Manula, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Kelvin Friday (Azam FC), Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Haroun Chanongo (Stand United) Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).

Mara baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini, kocha wa Stars Nooij aliwapa mapumziko ya siku 10, wachezaji waliokua kwenye michuano ya Cosafa mpaka Juni Mosi ambapo ndipo watajumuika na wachezaji wengine waliopo kambini.

Ifikapo Juni Mosi, 2015 Taifa Stars itaanza kambi ya moja kwa moja kujiandaa na mechi dhidi ya Misri itakayochezwa jijini Alexandria katika uwanja wa Borg El Arab Juni 14, 2015 ikiwajumuisha pia wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.

Kabla ya kuelekea nchini Misri, Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 4, Juni 2015 kwa muda wa wiki moja kabla ya kuelekea nchini Misri kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.

Juni 20, 2015 Taifa Stars itawakaribisha Uganda kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, zitakazofanyika nchini Rwanda 2016, na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili nchini Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.