Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-Kombe la dunia

Korea Kusini: pendekezo la kujiuzulu la kocha Hong Myung-bo lafutiliwa mbali

Shirikisho la soka nchini Korea Kusini (KFA) limetangaza alhamisi hii kwamba limetupilia mbali pendekezo la kujiuzulu kwa kocha wa timu ya taifa ya Korea Kusini, Hong Myung-bo, aliyolitoa baada ya timu yake kuondolea katika mashindano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Korea Kusini,Kim Shin-wook akikata tamaa timu yake kuendelea baada ya refa kupuliza kipenga cha mwisho.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Korea Kusini,Kim Shin-wook akikata tamaa timu yake kuendelea baada ya refa kupuliza kipenga cha mwisho. REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

“Tumeamua kuendelea kua na imami na Kocha wetu na tutaendelea kumuunga mkono”, naibu rais wa shirikisho la soka KFA, Huh Jung-moo ameambia vyombo vya habari mjini Seoul.

Huh amebaini kwamba kocha huyo alichukua na fasi ya mtangulizi wake Choi Kang-hee, mwezi juni uliyopita, huku akisema kwamba ataendelea kuinoa timu ya taifa ya Korea Kusini hadi utakapomalizika mkataba wake, ambao utafikia tamati baada ya kombe la Asia mwaka 2015.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Korea Kusini na kocha wao, walishushia lawama nchini Korea Kusini kwamba hawakufanya vizuri katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini brazil. Timu hiyo ya taifa ilimaliza ikiwa ya mwisho katika kundi H, baada ya kutoka sare na Urusi, huku mechi zake za awali ikiwa ilishindwa kufanya vizuri ilipocheza na Algeria pamoja na Ubelgiji. 

Mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria wakishangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Korea Kusini.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria wakishangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Korea Kusini. AFP / Javier Soriano

Hong, mwenye umri wa miaka 45, alikua beki mahiri wa timu ya taifa ya Korea Kusini ambayo ilifaulu kuingia katika robo fainali katika kombe la dunia la mwaka 2002.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.