Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Italia

Imeshiriki mara 17, imetwaa taji hili mara 4, iko katika nafasi ya 9 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.Wakiwa wamefanikiwa kutwaa mataji manne ya kombe la dunia mwaka 1934, 1938, 1982 na 2006 na kuwa washindi wa pili kwenye fainali za mwaka 1970 na 1994, timu ya taifa ya Italia maarufu kama “Azzurri”, ni ya pili kwenye orodha ya FIFA ya timu zilizopewa tuzo ya heshima ya bodi shirikisho hilo. Italia ni timu pekee ambayo inajumuishwa na Brazil kufanikiwa kutwaa kombe hili mara mbili mfululizo. Nusu fainali ya mwaka 1970 kati yake na Ujerumani inachukuliwa kuwa moja kati ya mechi zilizowahi kuwa bora zaidi toka kuanzishwa kwa mashindano hay. 

Timu ya Taifa ya Italia
Timu ya Taifa ya Italia fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Italia iko kwenye kundi D ikijumuishwa na timu za taifa za Uingereza, Costa Roca na Uruguay, hili ni moja kati kundi gumu kabisa kwenye michuano ya mwaka huu.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Mmoja ni mlinda mlango mkongwe na nahodha wa kikosi cha Azzurri, Gianluig Buffon ambaye amekuwa kwenye kikosi toka mwaka 2006 ambapo wenzake wengine walitemwa akijumuika pamoja na kiungo mkongwe Andrea Pirlo. Viungo makinda kama Andrea Ranocchia na Marco Verratti ni wachezaji wengine wanaopewa nafasi, wengine ni pamoja na Stephan El Shaarawy, Giuseppe Rossi, Mario Balotelli na Pablo Osvaldo ni wachezaji mahiri watakoleta chachu ya ushindi kwa timu hii.

Benchi la Ufundi.

Timu hii inaongozwa na kocha mkuu Cesare Prandelli.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Ni pamoja na kushinda taji hili mwaka 1934 nchini mwake, na kushinda tena mfululizo mwaka 1938 nchini Ufaransa, pia wakashinda taji hili mwaka 2006 nchini Ujerumani na mwaka 1982 nchini Uhispania, wameshinda pia taji la Olympic mwaka 1936 nchini Ujerumani.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Dino Zoff, Paolo Maldini na Silvio Piola

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.