Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Costa Rica

Imeshiriki mara 3, haijawahi kutwaa taji hili, katika nafasi ya 34 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Costa Rica, kwa mara ya kwanza timu hiyo ilicheza mchezo wake wa awali kabisa mwaka 1921 na kushinda kwa mabao 7-0 dhidi ya El Salvador. Baada ya miaka mingi ya kujaribu hatimaye walifanikiwa kucheza kombe la dunia mwaka 1990 wakipata nafasi baada ya Mexico kuondolewa na kufika fainali nchini Italia. Walifanikiwa kucheza fainali nyingine mwaka 2002 baada ya kushindwa kucheza fainali za mwaka 1994 kule Marekani. 

Timu ya Taifa ya Costa Rica
Timu ya Taifa ya Costa Rica fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Costa Rica iko kwenye kundi D ikijumuishwa na timu za taifa za Uruguay, Uingereza na Italia hili ni kundi la kifo kwa mujibu wa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya soka.

Wachazaji wa kuangaliwa.

“ the valiant Ticos” inawategemea wachezaji wake kama Bryan Ruiz, Alvaro Saborio, Cristian Bolanos na mlinda mlango Keilor Navas ni wachezaji ambao wanategemewa kwa sehmu kubwa kuleta mabadiliko kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Costa Rica.

Benchi la Ufundi.

Timu hii inaongozwa na kocha mkuu, Jorge Luis Pinto.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Kushiriki kombe la dunia mwaka 1990 nchini Italia na kuishia kwenye hatua ya 16 bora na pia kumaliza kwenye nafasi ya nne kwenye michuano ya kombe la dunia kwa vijana mwaka 2009 nchini Misri.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na, Hernan Medford, Paulo Wanchope na Walter Centeno

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.