Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Colombia

Imeshiriki mara 4, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 4 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.“Los Cafeteros” ukiondoa fainali za mwaka 1990 zilizofanyika nchini Italia wakati wa kizazi cha akina Rene Higuita na Carlos valderrama, timu ya taifa ya Colombia haijawahi kuvuka kwenye hatua ya makundi kwenye fainali zote tatu ilizowahi kushiriki. 

Timu ya Taifa ya Colombia
Timu ya Taifa ya Colombia fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Colombia iko kwenye kundi C pamoja na timu za Ugiriki, Ivory Coast na Japan, kundi hili sio gumu sana licha ya kuwa lolote linaweza kutokea.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Colombia pia inawachezaji ambao wanauwezo mkubwa wa kuyoa mchango wao kwenye timu lakini huenda Colombia ikamkosa mshambuliaji wake Radamel Falcao ambaye ni majeruhi na anakipiga na klabu ya Monaco ya Ufaransa. Timu hii inaongezewa uzoefu na walinzi kama Mario Yepes na Luis Perea, viungo ni pamoja na James Rodriguez na mfungaji Teo Gutierrez.

Benchi la Ufundi.

Timu ya taifa ya Colombia inaongozwa na kocha mkuu, Jose Pekerman.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Mafanikio ambayo Colombia imewahi kupata ni kama yale ya mwaka 2003 kwenye fainali za kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 kwenye falme za kiarabu na kumaliza ya tatu. Pia ilimaliza kwenye kumi na sita bora kwenye fainali za kombe la dunia la mwaka 1990.

Wachezaji Waliovuma.

Ni pamoja na Rene Higuita, Carlos Valderrama na Faustino Asprilla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.