Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Oscar Pistorius atarajiwa kutoa utetezi wake dhidi ya kesi ya mauaji inayomkabili juma lijalo

Mwanariadha mwenye ulemvu Oscar Pistorius anatarajiwa kusimama kizimbani kutoa utetezi wake wakati kesi yake ikianza tena wiki hii kwa kusikiliza upande wa utetezi unaotegemea uchunguzi wa wataalam kueleza ni kwa namna gani na kwa nini alimwua kwa risasi mpenzi wake. 

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa mahakamani, februari 20 mwaka 2013.
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa mahakamani, februari 20 mwaka 2013. afp
Matangazo ya kibiashara

Shahidi wa kwanza upande wa utetezi siku ya Jumatau atakuwa Jan Botha, mwanapatholojia mwakilishi wa Pistorius, kwa mujibu wa Brian Webber, mmoja wa wanasheria wa mwanariadha huyo.

Mahakama itaanza tena kusikiliza kesi hiyo baada ya Jaji Thokozile Masipa kuahirisha kesi hiyo ya mauaji kwa wiki nzima baada ya mmoja wa wazee wa baraza lake, msaidizi wa mahakama, kuugua.

Pistorius huendaakawa wapili kutoa utetezi wake baada ya Botha, na itakuwa mara ya kwanza kwake kuzungumza hadharani tangu mauaji hayo, badala ya kueleza kuwa hana hatia, na kutoa majibu ya ndio mara kwa mara kwa jaji Masipa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.