Pata taarifa kuu
MICHEZO

Timu ya Nkana yabanwa mbavu nyumbani michuano ya CAF

Matumainiya timu ya Nkana ya nchini Zambia kufuzu katika ya hatua ya makundi kwenye mashindano ya ligi ya Mabingwa barani Afrika CAF yamezama baada ya kujikuta ikibanwa mbavu nyumbani jana Jumamosi na timu ya Zamalek ya Misri. 

Mtanange kati ya Nkana ya Zambia na Zamalek ya Misri
Mtanange kati ya Nkana ya Zambia na Zamalek ya Misri afp
Matangazo ya kibiashara

Timu hiyo bingwa mara tano wa michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ilijikuta ikilazimika kwenda sare tasa na watani wake wa jadi timu ya Zamalek kwenye dimba la Nkana huko Kitwe.

Hii ni mara ya tatu mfululizo ambapo timu ya Nkana inakutana na Zamalek na kumalizika kwa msuguano ingawa mara zote Wamisri wameibuka washindi katika mechi zao za nyumbani na kusonga mbele dhidi ya wapinzani wao Zambia.

Jana Jumamosi, Nkana ilianza kwa kutawala mchezo na kuiwekea shinikizo timu ya Zamalek lakini hata hivyo timu hizo zikaambuia sare tasa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.