Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Bosi wa Cardif City amtaka kocha mkuu wa timu hiyo ajiuzulu mwenyewe ama afutwe kazi

Uongozi wa klabu ya Cardif City inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza umeelezwa kumuandikia barua kocha mkuu wa timu hiyo, Malky Mackey ikimtaka ajiuzulu nafasi yake ama afutwe kazi na bosi wa timu hiyo, Vincent Tan.

Kocha wa Cardif City, Malky Mackey akiwa na mmiliki wa klabu hiyo, Vicent Tan
Kocha wa Cardif City, Malky Mackey akiwa na mmiliki wa klabu hiyo, Vicent Tan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye barua yake iliyonaswa na vyombo vya habari nchini Uingereza, imemnukuu Tan akieleza kutoridhishwa kwake na mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanywa na kocha huyo ikiwemo masuala ya fedha na mfumo wa uchezaji.

tajiri huyo raia wa Malaysia ameingia kwenye mzozo na kocha wake baada ya kocha huyo juma moja lililopita kunukuliwa akisema kuwa anatumaini kuwa uongozi wa klabu hiyo utatoa fedha za kumuwezesha kusajili baadhi ya wachezaji.

kauli hiyo ilionekana kumkwaza tajiri huyo ambaye toka awali alishamweleza Mackay kuwa asitegemee kupata fedha zaidi kwaajili ya kufanya usajili wa wachezaji watakaoongeza nguvu kwenye timu yake wakati wa msimu wa dirisha dogo la usajili.

Akihojiwa kwenye chombo kimoja cha habari nchini humo, Mackay mwenyewe amesisitiza kutong'atuka kwenye nafasi yake licha ya kutofautiana na uongozi wa klabu yake.

Tan alionesha kuchukizwa na kauli ya Macky kutaka kufanya usajili mpya wakati wa dirisha dogo la usajili la mwezi January mwakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.