Pata taarifa kuu
Michezo-Football

Matayarisho ya CECAFA yazinduliwa Zambia

Mwalimu wa Zambia, Patrice Beaumelle, amewaalika wachezaji 27 kwenye kambi ya mazoezi kama sehemu ya matayarisho yao ya kushiriki Kombe la Cecafa nchini Kenya.

Mwalimu wa Zambia, Patrice Beaumelle
Mwalimu wa Zambia, Patrice Beaumelle mtnfootball.com
Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao wa Afrika wa 2012 watashiriki kama taifa alikwa kwenye shindano hilo linalojumuisha nchi za Afrika mashariki na kati ambalo litaguswa kutoka Novemba 27 hadi Desemba 12.

Zambia wako kwenye Kundi B pamoja na Burundi, Somalia na Tanzania huku wakimenyana kwanza na Tanzania Novemba 28 kabla ya kupatana na Burundi Desemba mosi.

Watakamilisha mechi za makundi dhidi ya Somalia Desemba 4.

Wachezaji walioalikwa walitakikana kuripoti Melsim Lodge jijini Lusaka Jumatano huku kambi hiyo ikifungwa Novemba 24.

Kati ya walioalikwa ni pamoja na kipa wa Zamcoal Diggers Charles Mutanga, nahodha wa kikosi cha mwaka huu cha Airtel Rising Stars Patson Daka anayechezea Kafue Celtic na mshambuliaji wa Kalulushi Modern Stars Shadreck Musonda.

Wengine ni Emmanuel Chimpinde na Lawrence Chungu wanaochezea Power Dynamos akiwemo pia Justin Zulu wa Kabwe Warriors.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.