Pata taarifa kuu
SOKA

Taifa Stars ya Tanzania yashindwa kufurukuta katika uwanja wa nyumbani baada ya kutoka suluhu na Zimbabwe

Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imetoka sare ya bila kufungana na timu ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa iliyopo katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA), iliyopigwa jana jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Kocha Mkuu wa Tanzani, Kim Poulsen, alilalamikiwa na mashabiki waliohudhuria mechi hiyo, kwa kushindwa kufanya marekebisho ya wachezaji walioshindwa kumudu mchezo.

Hata hivyo, Kipa Ivo Mapunda ambaye kwa muda mrefu hajaitumikia Taifa Stars alionekana kufanya vizuri langoni kwake na kuinusuru Stars kufungwa.

Kwa upande wake Zimbabwe ilitumia wachezaji wengi chipukizi huku Taifa Stars ikiwatumia wachezaji watano wanaocheza soka la nje ya nchi.

Awali Taifa Stars ilitakiwa kucheza na Harambee Stars ya Kenya, lakini Shirikisho la soka nchini Kenya FKF lilituma taarifa likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.