Pata taarifa kuu
football

TP Mzembe ya DRCongo kumenyana na Stade Malien katika mechi ya nusu fainali ya pili kuwania taji la shirikisho barani Afrika

Klabu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Jumamosi itamenyana na klabu ya Stade Malien katika mchuano wa nusu fainali ya pili kuwania taji la shirikisho barani Afrika.

TP Mazembe's Mulota Kabangu akisherehekea bao
TP Mazembe's Mulota Kabangu akisherehekea bao
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo utachezwa mjini Lumbumbashi kuanzia saa kumi na nusu saa za Afrika ya Ktai mchuano ambayop TP Mazembe watakuwa dimbani wakiwa wanaongoza kwa mabao 2 kwa 1 kutokana na ushindfi wao wa mzunguo wa kwanza wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo, gumzo kubwa mjini lubumbashi kwa sasa ni kukosekana kwa wachezaji wa Zambia wanaoichezea timu hiyo Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala baada ya serikali ya Lusaka kuwazuaia kurudi DRC kuichezea klabu yao.

Serikali ya Zambia ilitoa agizo la kukamatwa kwa wachezaji hao baada ya kutoichezea timu yao ya taifa katika mchuano wa kirafiki wa kitaifa dhidi ya Brazil katikatika ya mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.