Pata taarifa kuu
Michezo-Football

Timu ya taifa ya Vijana ya Ufaransa yashuka dimbani kumenyana na Irland kuka tiketi ya kucheza michauno ya Euro 2015

Timu ya taifa ya Ufransa ya vijana inashuka dimbani leo Jumatatu Octoba 14 kumenyana na Irland ambayo inakuja juu ya Ufaransa kwa pointi katika kuwania kufuzu kombe la Ulaya mwaka 2015. Iwapo Ufaransa itashinda mechi hiyo itachukuwa nafasi ya kwanza katika kundi hilo.

Geoffrey Kondogbia na Florian Thauvin
Geoffrey Kondogbia na Florian Thauvin Equipe
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Ufaransa ya vijana inaendelea na kampeni ya kutafuta tiketi ya kuwania kufuzu kombe la Ulaya mwaka 2015. Timu hiyo imeonyesha mafaanikio katika kampeni hizo baada ya kuichapa Armenia mabao 4-1 alhamisi iliopita.

Timu hiyo inasaka pointi jioni hii wakati itapo menyana na Irland ilio juu kwa pointi tatu zaidi ya Ufaransa na ambayo inakiporo cha mechi moja.

Wachezaji hao wanaongozwa na kocha  Willy Sagnol wanaelekea kujikatia tiketi ya kufuzu kwenye michuano hiyo ya kombe la Ulaya mwaka 2015.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.