Pata taarifa kuu
Kriketi

Tendulkar kustaafu kuichezea India mwezi Novemba

Mchezaji wa Kimataifa wa mchezo wa Kriketi kutoka nchini India Sachin Tendulkar ambaye amelichezea taifa lake miaka 24 michuano mbalimbai ya Kimataifa ametangaza kuwa atastaafu baada ya mchuano wake wa Kimataifa wa 200 dhidi ya West Indies mwezi Novemba mwaka huu utakaochezwa nyumbani.

Matangazo ya kibiashara

Tendulkar mwenye umri wa miaka 40 ameliandikia Baraza la Mchezo wa Kriketi nchini humo na kulifahamisha kuwa atastaafu na kueleza kuwa katika maisha yake yote alitamani kuichezea India ndoto ambao ameeleza imetimia ndani ya miaka 24 ambayo amekuwa akicheza mchezo huo.

Tendulkar ni mchezaji anayeenziwa sana nchini India na anaingia katika vitabu vya historia kuwa mchezaji wa pekee ambaye amewahi kulichezea taifa lake mechi nyingi ndani ya miaka 24 ambayo amekuwa akisafiri katika mataifa mbalimbali duniani kuiwakilisha India.

Mashabiki wa mchezo huu nchini India wamekuwa wakitarajia kustaafu kwake baada ya kutangaza kustaafu kushiriki katika michuano ya siku moja ya Kimataifa ya ODIs mwaka 2012.

Tendulkar atakumbukwa na wapenzi wa mchezo huu nchini India kwa kuwa katika kikosi cha wachezaji walioishindia India kombe la dunia mwaka 2011 na wakati wa kombe la dunia mwaka 2003 lililofanyika nchini Afrika Kusini, alitangazwa kuwa mchezaji bora.

Baraza la mchezo wa Kriketi nchini India linasema kuwa haliamini kuwa Tendulkar hataicheizea tena timu ya taifa baada ya mchuano wa mwezi Novemba.

Tendulkar anaingia katika rekodi ya mchezaji ambaye ameicheizea nchi yake mechi nyingi za Kimataifa katika historia ya mchezo huu tangu aanze kucheza mwaka 1989 na kuwa katika kikosi cha kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.