Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

TP Mazembe yaandikisha ushindi nchini Mali kutafuta ubingwa wa CAF

Rainford Kalaba na Tresor Mputu wa klabu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliipa timu yao ushindi dhidi ya Stade Malien ya Mali katika mchuano wa nusu fainali ya kwanza kuwania taji la shirikisho barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

TP Mazembe ambayo haijawahi kushinda taji hilo, ushindi wake wa mabao 2 kwa 1 ugenini umewapa matumaini ya kufika hatua ya fainali ikiwa watapata sare yoyote katika mchuano wa mzunguko wa mwisho wiki mbili zijazo jijini Lubumbashi.

Mshambulizi wa Stade Malien Morikaman Koita, ndiye aliyeifungia klabu yake bao la kufuta machozi na sasa watakuwa na kibarua kigumu mjini Lubumbashi wiki mbili zijazo kwa sababu wanastahili kuishinda TP Mazembe angalau mabao mawili kwa bila ili kutinga fainali.

TP Mazembe ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao la ufunguzi katika dakika ya 14 ya mchuano huo, kabla ya kupata bao la pili katika dakika ya 23 ya mchuano huo na kuwaacha mashabiki wa Stade Malien na huzuni kubwa hata kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Mashambulizi ya Stade Malien hayakuzaa matunda ya kuwapa ushindi lakini walipata bao la kuwasazisha katika dakika nne baada ya kufungwa mabao yote mawili bao ambalo liliwapa matumaini mashabiki wa nyumbani.

Mshindi wa mzunguko kati ya TP Mazembe na Stade Malien atamenya na Bizertin FC au Sfaxien FC zote kutoka Tunisia ambazo zilitoka sare ya kutofungana.

Katika michuano ya nusu ya fainali ya kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, Coton Sport ya Cameroon wakiwa nyumbani walitoka sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri.

Mchuano huo uliahirishwa kwa siku moja zaidi kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha Jumamosi iliyopita.

Katika mchuano mwingine, Orlando Pirates ya Afrika Kusini ilitoka sare ya kutofungana na mabingwa wa mwaka 2011 Esperence ya Tunisia.

Michuano ya pili ya nusu fainali itachezwa baada ya wiki mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.