Pata taarifa kuu
FIFA

Tom Saintfiet wa Malawi kumshtaki Stephen Keshi wa Nigeria FIFA

Kocha wa Timu ya soka ya Malawi Mbelgiji Tom Saintfiet amesema atamshtaki kocha wa Nigeria Stephen Keshi katika shirikisho la soka duniani FIFA kwa tuhma za kumtamkia maneno ya ubaguzi wa rangi.

Kocha wa timu ya soka ya Malawi Mbelgiji Tom Saintfiet
Kocha wa timu ya soka ya Malawi Mbelgiji Tom Saintfiet
Matangazo ya kibiashara

Saintfiet anasema Keshi amemwita “mtu mweusi anayestahili kurudi nchini Ubelgiji” matamshi ambayo kocha wa  Malawi anasema yamemuumiza na ni ya kibaguzi.

Mbelgiji huyo ameimbia idhaa ya michezo ya Uingereza ya  BBC kuwa tayari mawakili wake wameanza mchakato wa kuwasilisha malalamishi  kwa FIFA ili hatua ichukuliwe.

Mzozo kati ya Saintfiet na Keshi ulianza kudorora siku chache baada ya chama cha soka nchini Malawi kukiandikia kile cha Nigeria kutaka mchuano wa kufuzu katika mzunguko wa mwisho wa kusaka tiketi ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao kuahirishwa kutoka mjini Calabar kwa sababu za kiusalama.

Nigeria hata hivyo inasema kuwa kutakuwa na usalama wa kutosha katika uwanja huo wa Calabar licha ya kuwepo kwa vitisho vya kutokuwa na usalama na tayari wameshaifahamisha FIFA.

Saintefiet anasisitiza kuwa ikiwa kweli FIFA inalenga kuadhibu visa vya ubaguzi wa rangi katika mchezo wa soka ni sharti Keshi achukuliwe hatua kwa kile anachokisema kuwa yeye hamkumtusi yeyote ila ombi lake lilikuwa ni mchuano huo kupelekwa katika uwanja mwingine.

Nigeria na Malawi watamenyana tarehe 7 mwezi Septemba mchuano ambao Nigeria wanahitaji sare ili kusonga mbele huku Malawi wao wakihitaji ushindi ili kufuzu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.