Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-MICHEZO

Hong Myung-Bo ateuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Korea Kusini

Shirikisho la soka nchini Korea Kusini limetangaza kwamba Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya taifa hilo Hong Myung-Bo ameteuliwa kukinoa kikosi cha Korea Kusini kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Hong Myung-Bo kocha mpya wa timu ya taifa ya Korea Kusini
Hong Myung-Bo kocha mpya wa timu ya taifa ya Korea Kusini
Matangazo ya kibiashara

Hong mwenye umri wa miaka 44 tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuchukuwa nafasi ya Choi Kan-Hee alieondoka juma lililopita baada ya timu hiyo kufaulu kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa mara ya nane mfululizo kwa tofauti ya ma bao, jambo ambalo lilimchkiza sana kocha huyo na kuamuwa kuondoka.

Hong amewahi kuichezea timu hiyo ya taifa na kushiriki mara nne michuano ya kombe la dunia tangu mwaka 1990 na kuwa kinara wa timu wakati alipokuwa nahodha alieifikisha timu hiyo katika nusu fainali mwaka 2002 wakati michuano hiyo ilipoandaliwa nchini humo na Japan.

Kocha huyo atakabiliwa na kibarua kigumu cha kurejesha uwiano na uaminifu kati ya wachezaji hao waliofuzu kutokana na tofauti ya ma bao dhidi ya Ouzbekistan huku wakishindwa kuwika nyumban dhidi ya Iran katika mechi yao ya mwisho ya kuwania kufuzu.

Hong alianza kuwa kocha msaidizi mwaka 2005 na 2007 , na kufaulu kutwaa medali ya shaba kwenye michuano ya Olympic mwaka 2010 na kuchukuw anafasi ya tatu katika michuano ya Olympic ya mwaka 2012 jijini London ikiwa ni medali ya kwanza ya Olypiki kwa kwa taifa hilo kwenye mpira wa miguu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.